Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameendelea kushusha maneno kwa chama kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya kufunguka hadharani kuwa hawakuwa na sera ambazo zingemfanya aendelee kubaki.
Staa
huyo ambaye kwa sasa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kurudi
kwake CCM hakumaanishi kama amehongwa kama watu wanavyoendelea kusambaza
habari hizo bali amekwenda kutokana na kuvutiwa na sera.
“Naomba
nieleweke kuwa dhamira yangu ya kubaki Ukawa ndiyo ilikuwa ikinisuta.
Nikiwa kama mmoja wa wasanii, nimevutiwa na sera za CCM hasa kwa upande
wa wasanii ambapo Mgombea Urais, Magufuli (John Pombe) alisema moja ya
sera zao ni kujali maslahi kwa wasanii na kuwafungulia mfuko maalum
utakaowashughulikia,” alisema Ray.


No comments:
Post a Comment