Thursday, August 13, 2015
TCRA Watoa ADHABU Kwa Kituo cha Televisheni cha ITV

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa adhabu ya onyo kali na kukitaka kituo cha ITV kuomba radhi mara mbili mfululizo kwenye taariifa zake za habari baada ya kukiuka sheria ya utangazaji nchini ya Mwaka 2005.
Friday, August 7, 2015
Mke wa Dk Slaa afunguka......Akana Kumfungia Mumewe Chumbani
Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuzungumza na kusema yupo salama, mke wake, Josephine Mushumbusi amekanusha tuhuma zilizozagaa kuwa ndiye aliyemshauri kiongozi huyo wa Chadema kujiuzulu na kumzuia kushiriki vikao muhimu vya chama.
Tetesi
hizo zilivuma kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya
Dk Slaa kutoonekana katika vikao muhimu vya Chadema na Ukawa, kuwa
Mushumbusi hakupendezwa na kitendo cha Lowassa kupitishwa kuwania urais
chini ya mwavuli wa Ukawa na badala yake alitaka Dk Slaa ndiye awe
mpeperusha bendera.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo ambazo Mushumbusi amezikanusha, aliamua
kumfungia ndani Dk Slaa kama moja ya mbinu za kumzuia asishiriki
shughuli za kichama, tuhuma ambazo amezikanusha.
“Bosi wako akija kukuomba ushauri utamsaidia, lakini akija akakuambia ameshafanya maamuzi unaweza kupingana naye?” alihoji Mushumbusi akianza kutoa maelezo yake na kuendelea:
“Wakati
wa vikao nilikuwa namwona (Dk Slaa) anachelewa kurudi kila siku, siku
moja akaja akaniambia uamuzi aliouchukua na mimi sikuwa na la kusema,
nikachukua shuka nikajifunika.”
Katika
mahojiano yake ya kwanza baada ya kuzagaa kwa tetesi hizo, Mushumbusi
pia alikana kumfungia Dk Slaa ndani ya nyumba, akisema wakati maneno
hayo yalipokuwa yanazagaa, alikuwa nje ya nchi na wala hakujua
kinachoendelea.
“Mwenyewe
najiuliza nini kinaendelea, siwezi kufanya kitu kama hicho. Nyumba
yangu ina milango miwili, nawezaje kumfungia mtu, tena mwanamume, hata
watoto siwezi kuwafungia. Kuna mambo mengine mwanamke huwezi kuyafanya
kwa mwanamume. Mwanamume ni mwanamume tu,” alisema.
Alisema
viongozi wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wanafika
nyumbani kwake na walikutana na Dk Slaa na kuzungumza naye... “Kama ningekuwa nimemfungia wangezungumza naye vipi?”
Mushumbusi alisema mwanamke anaweza kufanya chochote lakini kuna baadhi ya mambo ambayo mwanamume akiamua ni vigumu kumzuia.
Akifafanua
tuhuma za kumshinikiza Dk Slaa kujiuzulu Chadema, Mushumbusi alisema
kiongozi huyo wa Chadema ana uamuzi wake na yeye ni msaidizi tu ambaye
hana uamuzi wa mwisho kwenye familia.
Hata
hivyo, alisema endapo angeamua kumshawishi, uwezo wa kufanya hivyo anao
lakini yeye ni mwanamke mwadilifu anayependa mafanikio ya mumewe.
“Kwani unanionaje? Mimi ni ‘strong’ (nina nguvu), ningetaka ningefanya hivyo, nisingeshindwa,” alisema.
Pamoja na hayo, Mushumbusi alilalamika kuwa tuhuma hizo dhidi yake zimesababisha asisikilizwe kama ilivyokuwa awali.
Bila
kufafanua kwa undani, alisema kuna kundi linalounda propaganda hizo ili
abadili mtazamo kuhusu mumewe lakini jambo hilo haliwezi kutokea.
“Nilisema
nitampenda kama alivyo, sitajali chochote wala akiwa katika hali gani
au chama gani. Kazi yangu ni kumtia moyo ili kile atakachofanya
kifanikiwe,” alisema.
Mbali
na kukanusha vikali tuhuma hizo, Mushumbusi alisema alikwishajitoa
kwenye masuala ya siasa kwa miaka miwili sasa na badala yake ameamua
kufanya biashara ya kuuza mkaa.
“Nimenyamaza
kimya, nimekaa kando ninaendelea na biashara yangu ya kuuza mkaa, nipo
mbali na siasa na sitaki kujua kinachoendelea, kwanza hata mchakato
wenyewe siujui,” alisema.
Aliwashauri
wanawake kuacha kushabikia masuala yanayotokea ndani ya ndoa yake na
kuwataka wavae viatu anavyovivaa na wajue kuwa anapitia wakati mgumu.
Wasomi Wampuuza Profesa Lipumba.......Wasema Amekurupuka
Wasomi mbalimbali nchini, wamepokea kwa mtazamo tofauti uamuzi wa Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu wadhifa wake wa Mwenyekiti wa CUF Taifa wengine wakisema suala hilo si jipya bali ni aina ya changamoto zilizopo kwenye vyama vya siasa nchini.
Wakizungumza
na mtandao huu kwa nyakati tofauti, wasomi hao pia walimshangaa Prof.
Lipumba kwa uamuzi huo kwani alishiriki tangu mwanzo katika kumpokea
mgombea urais aliyepitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Bw.
Edward Lowassa, tangu alipohama CCM na kujiunga na CHADEMA.
Dkt. Lazaro Swai wa OUT
Akizungumzia
uamuzi huo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na Jamii katika Chuo Kikuu
Huria Tanzania (OUT), Dkt. Lazaro Swai, alisema anamshangaa Prof.
Lipumba kwa uamuzi aliouchukua.
"Hizo
ni aina ya changamoto zilizopo kwenye vyama vya siasa tangu
vilipoanzishwa, hilo ni shinikizo kutoka upande mmoja lakini si kutoka
UKAWA wala CUF," alisema Dkt. Swai.
Aliongeza
kuwa, hivi sasa katika vyama vya siasa kila mtu ana mvuto wa aina yake
lakini kujiuzulu kwa Prof. Lipumba kutakuwa na mtikisiko kwa UKAWA na
CCM kutokana na kuhama kwa Bw. Lowassa.
"Ujio
wa Lowassa hauwezi kuipasua UKAWA, kujiuzulu kwa Lipumba kuna kitu
ndani yake na kuleta mashaka kwa Watanzania, kwanini iwe sasa ndipo
ajiondoe katika nafasi hiyo wakati alishiriki tangu mwanzo kumpokea
Lowassa," alihoji.
Askofu Bagonza
Askofu
wa Kanisa Katoliki Jimbo la Karagwe, mkoani Kagera, Benson Bagonza,
alisema kujiuzulu kwa Lipumba kunaashiria kuna jambo nyuma ya pazia,
kwani wananchi hawataelewa.
"Tangu
mwanzo alikuwa msingi imara kwenye UKAWA, ghafla anajiuzulu hiyo
inashangaza watu wengi na sitaki kuamini kama amefikia uamuzi huo," alisema na kuongeza;
"Kutakuwa
kuna jambo jingine limetokea nje ya UKAWA lakini swali la kujiuliza,
kwanini alichelewa kuchukua uamuzi huo...huyo si Lipumba tunayemjua," alisema.
Dkt. Benson Bana
Naye
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idara ya Sayansi ya
Siasa ya Jamii, Dkt. Benson Bana, alisema kujiuzulu kwa Prof. Lipumba
kulitarajiwa kutokana na mvutano uliokuwepo tangu awali.
"Ameona ni wakati mwafaka kuachia ngazi pia ni haki yake ya msingi kwani ndani ya muungano wa UKAWA, hauwezi kumpokea mtu wakati huo huo akawa maarufu kushinda chama.
"Hilo
ni pengo la kudumu ambalo haliwezi kuzibika kwa siku moja, uamuzi wa
Lipumba na Slaa utakuwa wa halali kwani waliwekeza sana kwenye vyama
vyao," alisema na kuongeza kuwa, kiongozi yeyote anapimwa kwa uadilifu na walikuwa tayari kujitoa kafara katika nyadhifa zao.
Julius Mtatiro
Kwa
upande wake, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Bw. Julius
Mtatiro, alisema hilo ni pigo kubwa kwa CUF na UKAWA hasa kipindi hiki
cha kutafuta ushindi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa ujumbe wake alioutuma kwenye akaunti yake ya Facebook, Bw.
Mtatiro alisema uamuzi huo ni mgumu kwani hajawahi kuusikia tangu awe
mwanachama wa CUF miaka nane iliyopita.
Alisema
kidemokrasia lazima kukubali matokeo na uamuzi binafsi wa mtu yeyote
kwani mwisho wa siku, mtu hufanya uamuzi wake na tunalazimika
kuyaheshimu ili maisha yaendelee.
Aliongeza
kuwa, si vizuri kumshutumu Prof. Lipumba kwenye mitandao na kwingineko
bali akumbukwe kwa mchango wake mkubwa kisiasa ambapo jemedari
anapoanguka vitani bunduki yake huchukuliwa na vita kuendelea.
Madiwani 18 wa CCM Wahamia CHADEMA
Madiwani
18 wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wametangaza kuhama chama hicho jana jijini Arusha.
Madiwani hao waliotangaza kuihama CCM walikuwa katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Arumeru.
Huku
aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elias Ngorisa aliyefuatana na
Diwani wa Kata ya Engusero Sambu, Kagil Mashati Ngukwo, ambaye pia
alikuwa Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Wilaya ya Ngorongoro naye pia
amejiunga na Chadema.
Walikuwepo
wazee wa mila wa Kabila la Wamasai (malaigwanani) Laurence Ngorisa na
Lekakui Oleiti, wote kutoka Engusero Sambu. Mbunge wa Arumeru Mashariki,
Joshua Nassari, ndiye aliyewapokea makada hao na kuwapatia kadi za
Chadema.
Akizungumza
baada ya kupokea kadi, Elias Ngorisa, alisema wapo madiwani 18 kati ya
28 ambao tayari wamechukua kadi za Chadema na kuondoka CCM na watatetea
nafasi zao kupitia Chadema katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.
Alisema
yapo mabadiliko makubwa na Watanzania hawana budi kuyakubali na
ameshawishika kubadilisha mwelekeo toka CCM kwenda Chadema.
Wednesday, August 5, 2015
Madereva watangaza mgomo mwingine nchi nzima
Mgomo mwingine wa madereva nchini Tanzania unanukia kufuatia Chama cha wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU pamoja na wizara ya kazi kushindwa kutekeleza makubaliano yayolifikiwa na tume iliyoundwa na waziri mkuu kutatua mgogoro huo.
Kwa mujibu wa naibu katibu mkuu wa TADWU, Bwana Rashidi Salehe
amesema kwamba kutokana na Wizara kushindwa kutekeleza makubaliano hayo
wanatarajia kugoma tena kuanzia Agosti tisa mwaka huu.
Amesema kuwa madereva watagoma tena kufuatia wizara ya kazi pamoja na Sumatra
kuendelea kutumia mikataba ya zamani katika kutoa leseni wakati
makubaliano ya tume iliyoundwa na waziri mkuu yalitaka mikataba mipya
ianze kutumika kuanzia julai mosi mwaka huu.
Katika makubaliano yao mapya, madereva wa
malori yanayotoka nje ya nchi walikuwa wanatakiwa kulipwa mishahara ya
shilingi milioni moja, huku madereva wa daladala shilingi laki tano
pamoja na posho.
Magufuli Alitikisa Jiji la Dar es Salaam Wakati Akichukua Fomu ya Kugombea Urais
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Cham cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo, ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.







Subscribe to:
Comments (Atom)












