Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameendelea kushusha maneno kwa chama kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya kufunguka hadharani kuwa hawakuwa na sera ambazo zingemfanya aendelee kubaki.
Staa
huyo ambaye kwa sasa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kurudi
kwake CCM hakumaanishi kama amehongwa kama watu wanavyoendelea kusambaza
habari hizo bali amekwenda kutokana na kuvutiwa na sera.




